SportsAZAM FC YAICHAPA NAMUNGO 2-1,DUBE ATUPIA Saleh4 years ago01 mins AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mchezo huo unemalizwa ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza baada ya mabao matatu kufungwa. Namungo FC walianza kutupia bao la kuongoza dakika ya 2 kupitia kwa Mohamed Issa likasawazishwa na Prince Dube dk ya 22. Bao la ushindi kwa Azam FC lilipachikwa dk ya 35 na Ismail Kader ilikuwa ni dk 35. Kipindi cha pili dakika 45 zilimeguka bila kupatikana bao na Azam FC kusepa na pointi tatu baada ya mchezo kukamilika. Azam FC inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya tatu na Namungo FC ipo nafasi ya nne na pointi 25. Post navigation Previous: VIDEO:HII HAPA ORODHA YA WACHEZAJI WALIOITWA STARS MTAZAME KOCHANext: BAO LA SAKHO LACHAGULIWA KUWA BAO BORA LA WIKI
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura Je Fainali ya Kombe la Dunia 2026 Itakuwa Brazil vs Hispania? Saleh24 hours ago 0