JURGEN Klopp,Kocha Mkuu wa Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England amethibitisha kwamba ataondoka ndani ya timu hiyo mkataba wake utakapomeguka 2024.
Ameongeza kuwa anaweza kuamua kubaki hapo ikiwa tu ataona ana nguvu ya kuweza kuiongoza timu hiyo.
Liverpool chini ya Klopp iliweza kuvunja mwiko wa kupitisha miaka 30 kusubiri taji la Ligi Kuu England akiwa amekaa hapo kwa muda wa miaka 6 na nusu.
Dili lake la mwisho kusaini ilikuwa ni 2019 Desemba amesema kuwa anapenda kile ambacho anakifanya.
“Ikiwa nitakuwa na nguvu kwa umuhimu bado nitakuwepo, ninanependa kile ambacho ninakifanya ,kuna vitu vingi vizuri ambavyo napata ikiwa ni pamoja na wachezaji wenye uwezo mkubwa na mzuri lakini siwezi kufikiria kuhusu hilo.
“Mimi nina nguvu lakini kwa uhakika kabisa sihitaji kukaa zaidi mpaka pale ambapo nitakuwa nimechoka kufikiria,”.