>

YANGA WAMTEMBELEA ALLY YANGA

UONGOZI wa Yanga jioni ya Machi 3,2022 waliweza kumtembelea mtoto Ally Kimara maarufu kama Ally Yanga ambaye ni shabiki wa Yanga na mchezaji ambaye anampenda ni Fiston Mayele.

Viongozi wa Yanga waliweza kufanya dua pia na Ally Yanga katika na kumuombea dua njema na kusema kuwa haitakuwa mwisho kutenda matendo ya huruma.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga aliomba dua na kumuombea afya njema mtoto huyo.

“Haitakuwa mwisho kwetu kuweza kufanya hivi na tunaomba kwa Mungu azidi kumlinda na kumpa afya njema. Tunaomba pia wachezaji wa Yanga wazidi kuwapa raha mashabiki na kupata ushindi ili kumpa furaha pia Ally,”.

Mayele amesema kuwa anamuombea dua mtoto huyo kwa kuwa anamapenzi na Yanga.

“Kwa kuwa yeye amesema anaipenda Yanga na sisi tunampenda pia, tunaombea kwa Mungu ampe afya njema,”.