>

WATATU SIMBA KUIKOSA BIASHARA UNITED LEO KWA MKAPA

NYOTA watatu wa kikosi cha kwanza cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco wanatarajiwa kuukosa mchezo wa leo wa ligi.

Simba ikiwa nafasi ya tatu inatarajiwa kumenyana na Biashara United Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa ligi wa mzunguko wa pili unaotarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.

Kwa mujibu wa Pablo ni Aishi Manula ambaye ni kipa namba moja, kiungo Sadio Kanoute pamoja na Taddeo Lwanga.

“Vijana wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Biashara United ni baada ya kurejea kutoka kwenye mashindano ya kimataifa na maandalizi yapo vizuri.

“Tutakosa huduma ya Manula ambaye ana matatizo ya kifamilia, Kanoute aliumia kwenye mchezo dhidi ya RS Berkane pamoja na Lwanga ambaye bado hajawa fiti,”.