>

RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO

NI mzunguko wa pili unaendelea na mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa leo Machi 4,2022.

Kagera Sugar v Namungo FC, Uwanja wa Kaitaba hii itapigwa saa 10:00 jioni.

Simba SC v Biashara United, Uwanja wa Mkapa hii itapigwa saa 1:00.

Kagera Sugar imetoka kupoteza mchezo wake mbele ya Yanga kwa kufungwa mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa hivyo wataingia wakiwa wametoka kujeruhiwa.

Simba wanakumbuka kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Karume waligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana hivyo watakuwa na kazi ya kujiuliza kwa mara nyingine tena.

Kwenye msimamo Simba ambao ni mabingwa watetezi wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 31 kibindoni.