MAKAMBO KUFUNGA YANGA BADO SANA APITISHA MECHI HIZI BILA KUFUNGA

HERITIER Makambo ndani ya Yanga amecheza mechi 11 kwa msimu wa 2021/22 bila kufunga kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ni namba moja kwenye safu ya ushambuliaji yenye mabao mengi ikiwa imetupia mabao 25 na mtupiaji namba moja ni Fiston Mayele mwenye mabao 7 na pasi mbili za mabao.

Kwa upande wa Makambo bado hajafunga bao baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Horoya alipokuwa baada ya kusepa Yanga alipocheza kwa msimu wa 2018.

Ndani ya ligi mambo yamekuwa bado magumu kwake kwa kuwa hajatupia wala kutoa pasi licha ya kupata muda wa kucheza katika kikosi kinachonolewa na Nasreddine Nabi ambaye ni kocha mkuu.

Katika mechi hizo 11 ambazo amecheza kati ya 15 zilizochezwa na Yanga ameyeyusha jumla ya dakika 290.

@dizo_click