FT:LIGI KUU:MTIBWA SUGAR 0-2 YANGA

UWANJA wa Manungu Complex mchezo umekamilika na ubao umesoma Mtibwa Sugar 0-2 Yanga.

Ni dakika ya 45+5 bao hilo lilipachikwa na kuwafanya Mtibwa Sugar wasiwe na chaguo la kufanya.

Mtupiaji wa bao la kuongoza ni Said Ntibanzonkiza ambaye ametumia pasi ya Feisal Salum.

Hakuna timu iliyoonyeshwa kadi ya nyekundu huku timu zote mbili zikicheza kwa mtindo wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

Fiston Mayele alipachika bao la pili kwa pasi ya Said ikiwa ni muda mfupi baada ya bao la Feisal kufutwa kwa tafsri kuwa alifunga kwa mkono.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 39 kibindoni huku Mtibwa Sugar ikiwa na pointi zake 12.