KOCHA AFUKUZWA,MRITHI WAKE KUANZA KAZI LEO

KICHAPO cha mabao 4-0 walichokipata Fountain Gate mbele ya JKT Tanzania katika mchezo wa Championship kimeotesha mbawa kibarua cha Ulimboka Mwakingwe aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo pamoja na kocha wa magolikipa Kibwana Nyongoli.

Mbali na benchi la ufundi pia kandarasi za wachezaji wawili zimesitishwa ikiwa ni kwa Tony Kavishe na Khalifa Mwande kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa iliyotolewa na Fountain Gate imeeleza kuwa ni Ahmed Soliman raia wa Misri atakuwa mrithi wa mikoba ya Ulimboka ambaye mkataba wake umesitishwa.

Kocha huyo mkataba wake unaanza kazi mara moja na atakuwa hapo kukamilisha mechi za mzunguko wa kwanza.

Leo Fountain Gate inatarajiwa kuwa na mchezo dhidi ya Kitayosce FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,Tabora.