SIMBA QUEENS YAPIGA KIFURUSHI CHA WIKI

SIMBA Queens imesepa na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya JKT Queens katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju.

Miongoni mwa waliotupja ni pamoja na Joel Bukulu ambaye alitupia bao moja kwa mkwaju wa penalti.

Pia Opa Clement alitupia mabao mawili katika mchezo wa leo na anafikisha mabao 17 kibindoni.

JKT Queens walicheza kwa nidhamu kubwa hasa katika safu ya ulinzi lakini walikosa wachezaji wao wazoefu kutokana na wengi wao kwenda masomoni.

Huu unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa Simba Queens Uwanja wa Simba Mo Arena kwa kuwa mchezo uliopita walishinda mbele ya Mlandizi Queens.