Home Sports PRISONS KUJIPANGA UPYA

PRISONS KUJIPANGA UPYA

BAADA ya jana kupoteza mbele ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu muhimu, Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons amesema kuwa watajipanga upya.

Kazumba Shaban amebainisha kwamba mpango wao ulikuwa ni kupata pointi tatu ila walipoteza mchezo huo kwa bao la penalti.

“Hesbu zetu ilikuwa ni kushinda mchezo wetu mbele ya Simba lakini tulipoteza kwa kufungwa bao 1-0 la penalti katika kipindi cha pili.

“Kipindi cha kwanza tulicheza mpira tukatengeneza nafasi lakini tukashindwa kufunga kwenye mchezo huo na kipindi cha pili tulicheza lakini hatukufunga.

“Tumepoteza mchezo wetu bado tuna kazi ya kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo tupo tayari hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema.

Prisons ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi 14 msimu wa 2021/22.

Previous articleCHEKI DAKIKA 360 ZA MOTO YANGA FEBRUARI
Next articleSIMBA QUEENS KUVAANA NA JKT QUEENS LEO