Dakika 45 Uwanja wa Mkapa timu zote hazijafungana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ubao unasoma Simba 0-0 Tanzania Prisons na timu zote mbili zinacheza kwa nidhamu kubwa hasa katika eneo la ulinzi.
Prisons madhambulizi yao ni ya kustukiza na wamepata kona mbili kuelekea lango la Simba huku Simba ikiwa imepata kona nne na zote hazijazaa matunda.
Mipira yote ya pembeni inayopigwa na Simba inaishia miguuni mwa mabeki wa Prisons.