RATIBA YA LIGI KUU BARA HII HAPA,YANGA KAZINI

LEO Jumapili, Januari 23,2022 vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanatarajiwa kuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 32 inakutana na Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu Malale Hamsini ikiwa na pointi 18.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi za timu hizo kuwa ngumu pale wanapokutana kwenye viwanja vya mkoani.

Mchezo wa mwisho uliochezwa Uwanja wa Ushirika,Moshi ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Pia mchezo mwingine leo ni kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya Namungo FC ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.