ABDULKARIM Amin,’Popat’ Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa wanatambua kwamba mchezo wao wa kesho dhidi ya Yanga utakuwa na ushindani mkubwa lakini wamejipanga kusaka ushindi. Kesho Januari 10 Yanga inatarajiwa kucheza na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi.
Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na mchezo wao uliopita walitoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya KMKM huku watupiaji wakiwa ni Heritier Makambo na Feisal Salum.