PABLO:TUMEAMUA KUWAPA FURAHA MASHABIKI WETU

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachagua kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo hivyo kesho watafanya vizuri kusaka ushindi.

Januari 10 Simba itakuwa na kibarua kwenye Kombe la Mapinduzi ambapo inatarajia kumenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Mchezo wake uliopita ilitoshana nguvu na Mlandege na dakika 90 zilikamilika kwa ubao wa Uwanja wa Amaan kusoma Simba 0-0 Mlandege.

Pablo amesema:”Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba timu ambayo tunakutana nayo inahitaji pia ushindi hamna namna lazima tuwe na mbinu ya kipekee.

“Kwetu utakuwa ni mchezo mgumu lakini tutajaribu kucheza mchezo wetu bora kwa sababu tumekuja hapa kuwapa furaha mashabiki,” ,

Bingwa mtetezi wa taji hilo ni Yanga yeye kesho anatarajiwa kumenyana na Azam FC kwenye hatua ya nusu fainali.