JEMBE JIPYA SIMBA LAANZA MAZOEZI RASMI

NYOTA Sharaff Shiboub tayari ameanza mazoezi rasmi na Klabu ya Simba kwa ajili ya kuweza kumpa nafasi Kocha Mkuu, Pablo Franco kuweza kumfanyia mchujo kama atamfaa.

Ikumbukwe kwamba Shiboub aliwahi kucheza Simba msimu wa 2019/20 ambapo Simba iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara na Ngao ya Jamii pamoja na Kombe la Shirikisho.

Anakumbukwa kwa kuweza kutupia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC hivyo kuna uwezekano akapewa kandarasi na kisaini dili la kuitumikia timu hiyo.

Habari zinaeleza kuwa hakusepa Simba kwa sababu ya kiwango kibovu bali kutokuwa na maelewano na kocha wa zama zile Sven Vandenbroec.

Jana Januari 3 baada ya kumtamvulisha Ofisa Habari mpya ambaye ni Ahmed Ally, Simba pia waliweza kutambulisha uzi mpya wa Kombe la Mapinduzi pamoja na Kombe la Shirikisho.