Home Sports KOCHA SIMBA ACHIMBISHWA

KOCHA SIMBA ACHIMBISHWA

IMEELEZWA kuwa Hitimana Thiery kocha msaidizi wa Simba amefikia makuliano ya kuachana na timu hiyo.

Kocha huyo alijiunga na Simba kwa ajili ya kuweza kuiongoza katika mashindano ya kimataifa kutokana na aliyekuwa kocha wa wakati huo Didier Gomes kutokidhi vigezo vya CAF.

Kwa sasa timu ya Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Pablo Franco mwenye ruhusa ya kukaa kwenye mechi za ushindani za kimataifa akiwa ameweza kuiongoza timu hiyo kwenye mechi za Kombe la Shirikisho.

Amefanikiwa kupenya na timu hiyo mpaka kwenye hatua ya makundi ambapo leo Desemba 28 makundi yamepangwa na timu ya Simba ipo kundi D ikiwa pamoja na timu ya RS Berkane ambapo mchezaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama anacheza.

Mtu wa karibu wa Hitimana Thiery amesema kuwa bado taarifa hazijafika rasmi kwenye meza ya kocha huyo lakini naye anaskia tu tetesi kwa sasa.

 

Previous articleJIONEE HAPA MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Next articleYANGA:LIGI NI NGUMU,TIMU ZOTE ZIMEJIPANGA