KMC YASAHAU KICHAPO CHA SIMBA,HESABU ZIPO HAPA

HABIB Kondo, Kocha Msaidizi wa Klabu ya KMC amesema kuwa wamesahau matokeo waliyoyapata mbele ya Simba sasa hesabu zao ni mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting.

KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kuwafanya wayeyushe pointi tatu mazima.

Leo KMC itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Matokeo ya mchezo wetu uliopita tumesahau kwa kuwa hayawezi kubadilika na badala yake tunautazama huu uliopo mbele yetu dhidi ya Ruvu Shooting.

“Hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi lakini ni muhimu kwetu kupata pointi tatu,” amesema.

KMC ikiwa imecheza mechi 10 imekusanya pointi 10 inakutana na Ruvu Shooting iliyokusanya pointi 9 baada ya kucheza mechi 10.