LEO Desemba 22 Ligi Kuu Bara inaendela huku mabosi wa Dar baada ya kutoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Mbeya City pale Azam Complex wana kibarua kingine tena.
Azam FC itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting hawa waze wa mpapaso,pira gwaride pira pasi, Uwanja wa Azam Complex.
Dakika 90 nyingine za nguvu itakuwa kwa Geita Gold kutoka migodini huko.
Ni Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro itakutana na Tanzania Prisons, Uwanja wa Nyankumbu.