>

SIMBA NDANI YA TABORA KUIVUTIA KASI KMC

KIKOSI cha Simba leo Desemba 22 kimewasili salama Tabora kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kuchezwa Desemba 24, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Ikiwa ipo nafasi ya pili na pointi 18 baada ya kucheza mechi 8 inakutana na KMC iliyo nafasi ya 9 na pointi 10.

Mchezo wa mwisho wa ligi KMC iligawana pointi mojamoja na Mtibwa Sugar katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Simba wao mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar uliahirishwa kwa kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wa Simba walikuwa wanaumwa mafua na homa.