YANGA INAONGOZA 3-0 IHEFU DAKIKA 45 KWA MKAPA

UWANJA wa Mkapa mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya tatu mchezo kati ya Yanga v Ihefu FC ni mapumziko.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inaongoza kwa mabao 3-0 na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa vifua mbele.

Watupiaji wa Yanga ni Heritier Makambo ambaye ametupia mabao mawili dk ya 5 na 22 huku lile la tatu likipachikwa na Khalid Aucho dk ya 45.

Bao la tatu pigo lake lilianza kwa Makambo na kipa wa Ihefu aliweza kulipangua mpira ukakutana na Aucho Uwanja wa Mkapa.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu ana kazi ya kwenda kujadili namna ya kupindua meza ni raundi ya tatu Kombe la Shirikisho.