MO AMETOA BILIONI 5.2 SIMBA MBALI NA ILE BILIONI 20

LEO Novemba 21, Klabu ya Simba imefanya Mkutano Mkuu na Wanachama ambao umefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambapo viongozi mbalimbali walikuwepo kwenye mkutano huo.

Akisoma ripoti ya fedha ya bajeti ya mwaka uliopita wa 2020,Mkuu wa Kitengo cha Fedha,Utawala na Uendeshaji, Yusuph Nassor amesema kuwa kwenye bajeti ya mwaka uliopita Mo amechangia bilioni 5.2.

“Kwenye bajeti ya mwaka uliopita Mohamed Dewji, Mo amechangia bilioni 5.2 ambayo ni kwa karibu na nusu bajeti ya Simba. Kipekee naomba tumpatie cheti cha shukrani. Hii ni nje ya ile bilioni 20.

“Kwenye bajeti ya msimu huu atatoa bilioni 5.1 na tayari ametoa bilioni 1.5 kati ya hizo billion 1.2 imetumika kwenye usajili,” amesema.

Pia kwa kutambua mchango wa Mo kwa kutambua mchango mkubwa ambao ameufanya  Klabu ya Simba kupitia kikao cha bodi kimeamua kumpa Urais wa heshima Mo.