>

YANGA YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA NAMUNGO

KIKOSI cha Yanga kimelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Ilulu.

Bao la Namungo limefungwa na Obrey Chirwa dakika ya 53 na bao la kusawazishwa kwa Yanga lilifungwa na Said Ntibanzokiza dk 82 kwa penalti.

Inakuwa ni sare ya kwanza kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na ni bao la penalti ambalo limewafanya wasepe na pointi moja leo.

Penalti hiyo imewafanya Namungo waweze kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu walionekana wakidai kwamba penalti haikuwa halali.

Alikuwa Jacob Masawe huyu alionyeshwa kadi ya njano na kadi nyekundu alionyeshwa Hamis Swaleh na kufanya Namungo kukamilisha dakika 90 wakiwa pungufu.

Yanga inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita huku kipa wake Diarra Djigui akibaki na clean sheet zake nne kwenye mechi sita kwa kuwa kwenye mechi mbili amefungwa bao mojamoja.