>

GEITA GOLD KITUO KINACHOFUATA KAITABA

BAADA ya Klabu ya Geita Gold kupoteza katika mchezo wake uliopita kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC, Novemba 20 wanakibarua kingine cha kusaka pointi tatu.

Kwenye mchezo huo Khoeminy Aboubakhari kipa wa Geita Gold aliweza kuokoa penalti ya matajiri wa Dar pale Azam Complex sasa kituo kinachofuata ni Kaitaba, Bukoba.

Geita Gold haijawa katika mwendo mzuri katika mechi zake tano za awali ambapo jambo hilo lilifanya iwe timu ya kwanza ndani ya ligi kumchimbisha kocha wao ambaye alikuwa ni Etienne Ndayiragije.

Kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Felix Minziro huku mchakato wa kumsaka kocha mpya ukiendelea kwa ajili ya kumpata mrithi wake.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 na pointi zake ni mbili inakutana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya tano na pointi 8.