Home Sports WAKIELEKEA KUIVAA RUVU SHOOTING, SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA MPYA

WAKIELEKEA KUIVAA RUVU SHOOTING, SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA MPYA

WAKIWA wanaelekea katika mxhezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting, tayari mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamemtambulisha kocha mpya mwingine.

Ni Don Daniel De Castro ambaye anakuwa kocha wa viungo akichukua nafasi ya Adel Zraine raia wa Tunisia ambaye alifutwa kazi Novemba 26 kutokana na timu hiyo kuboronga katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 mbele ya Jwaneng Galaxy ya Botswana ikiwa ni kipigo kikubwa kukipokea wakiwa Uwanja wa Mkapa mbele ya mashabiki wao ambao walikuwa wanaamini kwamba timu hiyo inatinga hatua ya makundi.

Pia hata kocha Didier Gomes naye alibwaga manyanga kutokana na timu hiyo kushindwa kufanya vizuri na kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Previous articleSAIDO V MAKAMBO KWENYE VITA MPYA YANGA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE