Home Sports SAIDO V MAKAMBO KWENYE VITA MPYA YANGA

SAIDO V MAKAMBO KWENYE VITA MPYA YANGA

UONGOZI wa Yanga baada ya kutangaza kuwa utamkosa mshambuliaji wake Yacouba Songne kwa zaidi ya miezi minne kutokana na majeraha aliyoyapata, mchezaji huyo ni kama ameacha vita ya namba kwa washambuliaji Saido Ntibazonkiza na Heritier Makambo kwa ajili ya kuchuana kuchukua nafasi ya mshambuliaji huyo.

Songne aliumia katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambapo katika mchezo huo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Uongozi wa Yanga tayari umethibitisha mchezaji huyo atapelekwa nchini Tunisia kwa matibabu akiambatana na daktari wa timu hiyo, Youssef Mohammed.

Katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting mara baada ya Yacouba kuumia, nafasi yake ilichukuliwa na Saido na akafanya vizuri.

Wakati huohuo pia kocha Nasreddine Nabi wa Yanga katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Mlandege ya Zanzibar, alionekana akitumia mfumo wa washambuliaji wawili wa mbele ambao ni Fiston Mayele na Heritier Makambo jambo ambalo ni tafsri huenda akaamua kumrudisha Makambo ndani ya Yanga katika michezo ijayo ya ligi kuu baada ya Yacouba kukosekana.

 

Katika mchezo huo wa kirafiki Makambo alifanikiwa kuifungia Yanga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 ilikuwa ni Novemba 9, Uwanja wa Amaan pia kwenye mchezo dhidi ya KMKM ni Fiston Mayele aliweza kufunga wakati timu ya Yanga ikishinda mabao 2-1 na lile lingine lilifungwa na Jesus Moloko.

Tayari kwa sasa Yanga ipo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mchezo ujao ni dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ilulu.

Previous articleDEAN SMITH APATA DILI JIPYA
Next articleWAKIELEKEA KUIVAA RUVU SHOOTING, SIMBA WAMTAMBULISHA KOCHA MPYA