DEMBELE AKATWA MKWANJA HUKO KISA DAKIKA TATU

OUSMANE Dembele, nyota wa kikosi cha Barcelona amekuwa wa kwanza kukutana na balaa la kocha mpya, Xavi Hernandez kisa kuchelewa kwenye mazoezi kwa muda wa dakika tatu pekee.

Kwa kosa hilo ambalo amefanya amekutana na ishu ya kukatwa mkwanja mrefu kwenye mshahara wake hivyo asitarajie kupewa mshahara wake kamili kwa mwezi huu kwa kuwa amesharikoroga huko.

Mkwanja huo ambao umekwata haujawekwa wazi hiyo ni kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo ikiwa ni sheria zake katika kutaka kurejesha nidhamu kwenye timu.

Xavi baada ya kutua Barcelona aliweka sheria 10 kwa wachezaji wake pamoja na wafanyakazi wenzake ili kuweza kuona kwamba mambo yanakwenda sawa na katika sheria hizo ambazo ameweka moja inaeleza kuwa mchezaji anatakiwa kuwa eneo la mazoezi dakika 90 kabla ya programu kuanza.