Home Sports YANGA YAACHANA NA KIUNGO MAZIMA

YANGA YAACHANA NA KIUNGO MAZIMA

YANGA imeachana na aliyekuwa nyota mpya ndani ya klabu hiyo ambaye alikuwa akisubiri dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kusaini mkataba mpya ambaye ni raia wa Ghana, Geofrey Nyarko.

Nyota huyo alijiunga na Yanga baada ya kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili akiwa mchezaji huru kwa ajili ya kufanya majaribio ndani ya kikosi hicho.

Nyarko ambaye anacheza nafasi ya winga, kwa mara ya kwanza alionekana kwenye kikosi wakati timu hiyo ilipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kwenye kikosi cha Nabi kilichoenda Zanzibar kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Mlandege (1-0) na KMKM kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Namungo, nyota huyo hakuwepo kwenye kikosi hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Ufundi wa Yanga, Dominick Albinus, alisema:“Mchezaji wetu ambaye alikuwa anafanya majaribio ameshaondoka kwenye timu hivi karibuni.

“Tumemruhusu kutokana na sheria za ligi ambazo zinaonyesha kuwa unaruhusiwa kusajili wachezaji 12 ila kwenye mechi wanaocheza ni nane tu, hivyo hata tukimsajili anaweza akakaa jukwaani, tumeamua kumwacha aende kwani tayari tuna wachezaji 10 wa kigeni.”

Chanzo:Championi

Previous articleDEMBELE AKATWA MKWANJA HUKO KISA DAKIKA TATU
Next articleAIR MANULA NA DAKIKA ZAKE BONGO