FEI TOTO:NAPENDA KUONA TIMU INASHINDA

FEISAL Salum, kiungo wa Yanga amebainisha kuwa jambo ambalo analipenda akiwa uwanjani ni kuona timu yake inashinda.

Fei ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ametupia mabao matatu na pasi moja kati ya tisa ambayo yamefungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Katika mechi tano ametumia jumla ya dakika 425 uwanjani akiwa ni miongoni mwa wazawa waliotumia dakika nyingi ndani ya uwanja katika kikosi cha Yanga.

Kiungo huyo amesema:”Napenda kuona timu inapata matokeo katika mechi ambazo tutacheza na hilo ni jambo ambalo kila mchezaji anahitaji kuona linatokea.

“Kufunga ama kutikufunga sio lazima iwe mimi tupo wachezaji wengi lakini jambo la msingi pointi tatu muhimu, “.

Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 15 kituo kinachofuata ni Namungo,  Uwanja wa Ilulu.