RUVU SHOOTING HESABU ZAO HIZI HAPA

 

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa ubora wa kikosi ambacho eanacho kwa sasa hawana wasiwasi na mechi za Ligi Kuu Bara.

Bwire amebainisha kuwa wanajivunia kutokana na kutumia kikosi kazi chenye wazawa huku wakiwa na malengo ya kufanya vizuri katika kila mechi.

“Tuna wachezaji wazuri ambao wana uwezo mkubwa na kila mchezaji malengo yake ni kuona timu inapata ushindi.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa kila kitu kinawezekana na kikubwa ni kupata matokeo mazuri,”.

Mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Yanga na kuziacha pointi tatu mazima Uwanja wa Mkapa.