WACHEZAJI wa Azam FC wameendelea na maandalizi ya mechi zao zijazo za Ligi Kuu Bara na chimbo lao likiwa ni palepale katika Uwanja wa Azam Complex.
Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina katika mechi tano ambazo ni dakika 450 imekusanya pointi 7 ipo nafasi ya nane na safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao manne.
Katika kujiweka sawa zaidi inatarajia kushuka uwanjani kwa mara nyingine tena Novemba 13 itakuwa dhidi ya JKU SC kutoka Zanzibar.
Mchezo huo utakuwa ni wa kirafiki kwa muda huu ambao ligi imesimama kupisha maandalizi ya timu ya taifa kushiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia, 2022 Qatar.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, ‘Zakazakazi’ ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kufanya vizuri kwenye mechi zao zote na kupata pointi tatu muhimu.
“Malengo yetu makubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote na kupata matokeo chanya hivyo mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi ni mwendo wa kimyakimya,”.