MADRID YAINGIA ANGA ZA CHELSEA

Real Madrid imetajwa kuwa ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota wa Chelsea, Antonio Rudiger ambaye ni beki wa kati.

 

Ikiwa dili lake litajibu basi mkwanja ambao atalipwa kwa wiki itakuwa ni pauni 200,000 na ni itakuwa kwa wiki jambo ambalo linaongeza urahisi katika kukamilisha dili hilo.

Madrid ipo tayari kuwauza wachezaji wake ili kumpata nyota huyo na wanaotajwa kuuzwa ni pamoja na Gareth Bale, Isco na Marcelo ili kukamilisha dili la nyota huyo.

Rudiger amekuwa kwenye ubora na timu kibao kwa sasa zinamtolea macho baada ya kuiongoza Chelsea kusepa na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na alitua hapo 2017 akitokea Roma kwa pauni milioni 29.