Home Sports HAJI MANARA AWAIBUA WAZAWA WA KAZI CHAFU

HAJI MANARA AWAIBUA WAZAWA WA KAZI CHAFU

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo wazawa wengi ambao wanafanya vizuri ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Shomari pamoja na Feisal Salum.

Nyota hao kwa sasa wana uhakika wa namba kikosi cha kwanza ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasredddine Nabi  huku nahodha akiwa ni mzawa pia Bakari Mwamnyeto.

Kwenye safu ya ulinzi Yanga ikiwa imecheza mechi nne haijaruhusu bao huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia jumla ya mabao sita na timu hiyo inaongoza ligi baada ya kufikisha pointi 12 na wanaopiga kazi chafu kwenye safu ya ulinzi ni pamoja na Job,Kibwana na Mwamnyeto huku kwenye upande wa viungo yupo Fei Toto.

Manara amesema:”Wapo wachezaji wengi ndani ya Yanga ambao wanafanya vizuri na kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati ndani ya kikosi cha Yanga.

“Yupo nahodha Bakari Mwamnyeto huyu sio beki tu bali ni nahodha pia ambaye anafanya kazi kubwa ndani ya uwanja, Kuna Kibwana Shomari hawa nao wanafanya kazi kubwa kwenye kikosi.

“Dickoson Job pia sasa kwa Yanga hii wachezaji wote ambao wanaanza ni bora na hata wale ambao wanakuwa benchi nao ni bora hivyo mashabiki mna kila sababu ya kutamba kwa ajili ya timu yenu,” .

Kesho Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 12:15 jioni.

Previous articleORODHA YA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA
Next articleRUVU SHOOTING:TUNA ASILIMIA NYINGI KUSHINDA MBELE YA YANGA