SIMBA YASHINDA MBELE YA POLISI TANZANIA

KIKOSI cha Simba leo Oktoba 27 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Bao la ushindi limefungwa na kiungo Rarry Bwalya dakika ya 89 kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na kiungo Bernard Morrison.
Kwenye mchezo wa leo Polisi Tanzania walikuwa kwenye ubora huku wakicheza soka safi sawa na Simba ambao wao walikuwa wakipambana kupata ushindi mapema ila mambo yalikuwa magumu.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza timu zote mbili zilitoshana nguvu na kwenda katika vyumba vya kubadiishia nguo wakiwa wametoshana nguvu kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 0-0 Polisi Tanzania.

Mpaka kipindi cha pili kinakamilika hapo ndipo Simba waliweza kupata ushindi kwa penalti hiyo iliyosababishwa na mchezaji wa Polisi Tanzania kwa mujibu wa mwamuzi wa kati.

Kwa matokeo ya leo Polisi Tanzania inashuka kutoka nafasi ya kwanza mpaka nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Yanga na Simba ipo nafasi ya tatu na ina pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu.