
SIMBA FANYENI KWELI LEO KIMATAIFA
SIMBA SC, leo Jumapili inatarajiwa kuvaana na ASEC Mimosas katika mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Saalam. Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba katika hatua hii ikiwa ni timu pekee ya Tanzania katika michuano hiyo. Simba imekuwa na historia nzuri katika michuano hiyo ya kimataifa kwa siku za karibuni, tunaamini kuwa wataendakufanya kweli kuanzia mchezo wa leo…