
LIVERPOOL WAKWAMA KUSEPA NA POINTI TATU DARAJANI
WAKIWA Uwanja wa Stamford Bridge, Liverpool ilikwama kusepa na pointi tatu mbele ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England. Watajilaumu wenyewe kwa kuwa walipata mabao ya mapema ndani ya dakika 30 za mwanzo kupitia kwa Sadio Mane dakika ya 9 na Mohamed Salah dakika ya 26. Hao Chelsea wanaonolewa na Thomas Tuchel walipindua meza…