
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar. Ikiwa ni namba moja katika msimamo na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 kituo kinachofuata ni Manungu. Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hawana hofu na mchezo huo kwa kuwa maandalizi yapo…
KAZI ya Mungu haina makosa na tunapaswa kumshukuru kwa kila jambo ambalo linatokea kwenye maisha yetu ya kila siku kwa kuwa yeye ni muweza wa kila kinachotokea. Hakuna ambaye anaijua kesho hivyo kwa muda ambao upo kwa wakati huu kila mmoja anajukumu la kutimiza yale yanayofaa bila kuchoka. Wanafamilia,ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu…
MTIBWA Sugar imethibitisha kuwa muda wowote kuanzia sasa, itaanza kumtumia winga wao raia wa DR Congo, Deo Kanda baada ya kila kitu kukamilika. Thobias Kifaru,Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa walikuwa wanashindwa kumtumia nyota huyo kwa sababu kuna vitu kuhusu uhamisho wake vilikuwa havijakamilika ila kwa sasa kila kitu kipo sawa. Ikumbukwe kwamba nyota…
HATUA kubwa ambayo mmefanya kwa ushindi kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa mnastahili pongezi wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho. Simba hamjafanya jambo dogo kwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas Uwanja wa Mkapa hakika mnastahili pongezi lakini ukweli ni kwamba kazi ndiyo kwanza inaanza. Vigongo ambavyo vinakuja kwenu ni vikubwa na…
KICHAPO cha mabao 4-0 walichokipata Fountain Gate mbele ya JKT Tanzania katika mchezo wa Championship kimeotesha mbawa kibarua cha Ulimboka Mwakingwe aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo pamoja na kocha wa magolikipa Kibwana Nyongoli. Mbali na benchi la ufundi pia kandarasi za wachezaji wawili zimesitishwa ikiwa ni kwa Tony Kavishe na Khalifa Mwande kwa makubaliano…
BAADA ya kucheza mechi 16 bila kupoteza ambazo ni dakika 1,440 Klabu ya DTB ilinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Green Warriors FC ambao waliweza kutibua rekodi hiyo katika mchezo wa 17 uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Februari 13 kwenye Championship. Wakati huu inajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya African Sports unaotarajiwa…
KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ametoa majukumu mazito kwa wachezaji wa timu hiyo, akiwemo kinara wa mabao, Fiston Mayele kwa kuhakikisha wanatupia mabao ya kutosha katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi. Nabi ametoa kauli hiyo baada ya kurejea kwa ligi kufuatia kumaliza mechi za Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) huku wakiwa na kumbukumbu za matokeo ya suluhu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City kabla ya ligi kusimama kupisha Shirikisho. Yanga inaongoza ligi ikiwa…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
OFISA Habari wa Simba, Ahmed Ally leo Februari 18 ameweka wazi kwamba wanakwenda Niger kusaka ushindi kwenye mechi za kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika.
FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga ameweka wazi kwamba anahitaji kusepa na tuzo za ufungaji bora kwenye mashindano yote ambayo anashiriki kwa msimu wa 2021/22. Kwenye ligi Mayele ametupia mabao sita akiwa ni kinara kwa upande wa Yanga na pia ametoa pasi mbili za mabao kwa upande wa Kombe la Shirikisho ametupia bao moja ilikuwa ni…
WAWAKILISHI wa Tanzania kimataifa katika Kombea Shirikisho, Simba leo wanatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Niger. Simba itakuwa na mchezo dhidi ya USGN ya Niger ambao ni wa makundi katika Kombe la Shirikisho. Mchezo wa kwanza wa Simba katika Kombe la Shirikisho walishinda mabao 3-1 ilikuwa dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Ni Shomari Kapombe,…
RAIS wa Makampuni ya GSM Group, Gharib Salim Mohammed, Jumapili aliwaalika mastaa wa Yanga nyumbani kwake Kigamboni, Dar es Salaam wakiongozwa na Fiston Mayele na Chico Ushindi kwa ajili ya kula chakula cha mchana sambamba na kufanya kikao kizito. Yanga ambao ni mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara wakibeba ubingwa huo mara 27 ikiwa…
MCHEZO wa KMC FC wa Ligi kuu ya NBC Soka dhidi ya Dodoma Jiji uliopangwa kuchezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jumapili ya Februali 20,2022 umehamishwa na sasa utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es Salaam saa moja kamili jioni. Kwa mujibu wa barua ya Bodi ya Ligi (TPLB) iliyotumwa jana mchana…
Ubora wa hali ya hewa umekuwa ukiongoza mijadala mikubwa ya masuala ya kimataifa kwa miongo kadhaa sasa. Ndio maana Meridian Gaming Group inafanyia kazi moja ya miradi mikubwa ya mazingira kwa sasa. Kampuni hii inafanya kazi katika masoko zaidi ya 30 Ulaya, LATAM na Afrika, inapanga kutoa zaidi ya miche 20,000 katika kila soko inaloendesha…
WACHEZAJI watatu tegemeo wa Simba, Chris Mugalu, Kibu Denis na Hassan Dilunga, wapo katika hatihati ya kuongozana na msafara wa timu hiyo utakaokwenda nchini Niger. Simba leo inatarajiwa kusafiri kuelekea Niger kuvaana na US Gendarmerie kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Jumapili hii. Katika michuano hiyo, Simba wapo Kundi D na timu za ASEC…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Ijumaa