
KIUNGO SAKHO HANA PRESHA KUHUSU YANGA
WINGA wa kimataifa wa Senegal anayecheza Simba, Pape Ousmane Sakho, amesema wala hana presha kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, huku akibainisha kwamba, anauchukulia mchezo huo kama mingine aliyowahi kucheza. Sakho ambaye amejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu, amekuwa moja ya wachezaji bora ndani ya kikosi hicho kutokana na kiwango alichokionesha…