
MUDATHIR YAHYA AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA YANGA
Kiungo wa kati wa Klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Mudathir Yahya Abbas, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani. Licha ya ofa ya kuvutia kutoka Azam FC – klabu aliyowahi kuitumikia kabla – Mudathir amechagua kubaki Yanga, akivutiwa na nguvu ya ushawishi wa Rais wa klabu…