
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE, MACHI 15,2022
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne, Machi 15,2022
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne, Machi 15,2022
KLABU ya Yanga kwa sasa ipo kwenye mchakato wa uchaguzi ambapo imeweka wazi kuwa kutakuwa na mfumo mpya utakaotumika katika upigaji kura. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Malangwe Mchungahela amesema kuwa yote hayo ni kutokana na mabadiliko ya katiba ambayo imepitishwa na wanachama. “Uchaguzi wa matawi unatakiwa kuanza Machi 18…
SHABIKI wa Simba, mzee Ulaya maarufu kama pasi milioni ameweka wazi kuwa mpira uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Simba 1-0 RS Berkane Machi 13 ulikuwa mkubwa na walistahili ushindi huku akitupa dongo kimtindo kwa watani zao wa jadi.
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ni miongoni mwa wale ambao walikuwa Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba v RS Berkane na aliweza kupeana salamu na mkono na Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally. Kwenye mchezo huo Simba ilishinda bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Pape Sakho dakika ya…
ANAANDIKA Saleh Jembe:- WAKATI Simba inapoteza 2-0 dhidi ya Berkane kule Morocco, Fiston Abdullazak alikuwa jukwaani kabisa. Wakati Simba ikishinda 1-0 pale kwa Mkapa dhidi ya Berkane, alipata bahati angalau ya kuwa benchi. Ajabu sana mchezaji huyu ambaye aliachwa na Yanga kutokana na kiwango duni alisajiliwa Berkane (Amini suala la bahati lipo), jiulize vipi timu…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
KIUNGO mshambuliaji tegemeo wa Yanga hivi sasa, Mrundi Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ ameondolewa kwenye mipango ya kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kwa muda wiki tatu kutokana na tatizo la goti. Hiyo itamfanya akose mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC utakaochezwa Machi 19, mwaka huu kwenye Uwanja Mkapa, Dar. Daktari wa…
UBAO wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 1-0 RS Berkane katika mchezo wa Kombe ma Shirikisho uliochezwa leo Machi 13. Ni mchezo ambao ulimalizwa na Simba kipindi cha kwanza kwa bao pekee la ushindi la Pape Sakho dakika ya 44. Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa awali uliochezwa Morocco, Berkane ilishinda kwa mabao 2-0. Florent Ibenge…
UWANJA wa Mkapa, mchezo wa kimataifa kati ya Simba v RS Berkane dakika 45 za awali zimemeguka. Ubao unasoma Simba 1-0,RS Berkane hivyo dakika 45 za kipindi cha pili zitaamua. Mtupiaji wa bao la kuongoza ni Pape Sakho ilikuwa dk ya 44 kwa shuti la mguu wa kulia akiwa ndani ya 18. Kutokana na kucheza…
KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amesema hakuna matokeo yoyote ambayo anayahitaji zaidi ya ushindi katika mchezo wa Kundi D dhidi ya RS Berkane. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema wanatarajia kuwa na…
KIUNGO wa Simba, Clautos Chama raia wa Zambia amesema anawahusudu sana baadhi ya wachezaji wa kigeni kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga. Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Chama amesema pia anawakubali pia wachezaji wenzie wakigeni kwenye timu ya Simba. “Nadhani nitawataja Pape Sakho, Peter Banda, Saido Ntibazonkiza, Aucho licha ya kuwa sijamtazama sana akiwa anacheza…
MASHABIKI wa Yanga Machi 12 waliweza kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa hisani uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Yanga dhidi ya timu ya Taifa ya Somalia ambao ulikamilika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1. Hivi ndivyo mashabiki waliweza kutoa heshima kwa Ally Kimara kabla ya mchezo kuanza:-
WAPINZANI wa Simba kimataifa RS Berkane ya Morocco walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuikabili Simba Uwanja wa Mkapa na miongoni mwa nyota ambao walikuwepo ni pamoja na Fiston Abdulazack na Tuisila Kisinda ambao waliwahi kucheza Klabu ya Yanga. Mchezo wa kwanza wa kundi uliochezwa nchini Morocco, Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo…
KWENYE mchezo wa Hisani uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kati ya Yanga dhidi ya timu ya taifa ya Somalia timu hizo mbili zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1. Bao la Somalia lilifungwa na Zakaria na bao la Yanga lilifungwa na kiungo Chico Ushindi ambaye alifunga bao hilo akitumia krosi ya Djuma Shaban. Mchezo huo ulihudhuriwa…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili
LEO Machi 12, kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane unaotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Mkapa.