
NABI AWEKA REKODI MPYA YANGA
BAADA ya kikosi cha Yanga chini ya Kocha Nasreddine Nabi kugotea kwenye mechi 49 mfululizo kucheza bila kupoteza katika Ligi Kuu Bara, kasi yao imekuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kushusha dozi kila wanayekutana naye, huku ikiaziacha mbali Simba na Azam. Ikumbukwe kwamba, Novemba 29, 2022 kwenye Uwanja wa Highland ubao uliposoma Ihefu 2-1…