
MASHABIKI WAJAA KWA WINGI MKAPA KUSHUHUDIA SIMBA DAY
Mashabiki wa Simba SC wamejitokeza kwa wingi muda huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, kushuhudia tukio kubwa na la kipekee la Simba Day. Hii ni siku maalum ambayo hutumika kuzindua kikosi kipya cha Simba kwa msimu mpya, kuwatambulisha wachezaji wapya, pamoja na burudani mbalimbali zinazochanganya muziki, michezo ya jukwaani na shamrashamra…