
SIMBA WAMFANYIA HAYA KIUNGO CHAMA
UKISIKIA watu wanakwambia Simba wamefanya kufuru, basi amini kwamba ufanikishaji wa kuipata saini ya kiungoMzambia, Clatous Chama imetumika gharama kubwa sana. Chama ambaye amerejea Simba na kusaini mkataba wa miaka miwili, aliondoka kikosini hapo Agosti 2021, baada ya kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2018/19 hadi 2020/21na kutua RS Berkane ya Morocco. Pia Chama alikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichocheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika…