BOSI wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa hatma ya mkataba wa winga wa timu hiyo Bukayo Saka itafahamika hivi karibuni.
Saka amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Arsenal ambapo kocha wa timu hiyo anapambana kusuka kikosi upya.
Winga huyo mkataba wake wa awali unamalizika Juni 2024 kikosini hapo.
Timu za Manchester United, Manchester City na Liverpool zinatajwa kumpigia hesabu nyota huyo.
Arteta amesema:”Ninaamini Bukayo, klabu pamoja na familia yake watakuwa wamefikia pazuri na kwa sasa kinachosubiriwa ni saini yake tu,” .