NABI:TUNAHITAJI UTULIVU KUSHINDA

NASREDDINE Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanahitaji utulivu mkubwa ili kuweza kushinda mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Taji hilo Yanga wanalitetea ambapo walishinda mbele ya Simba kwa bao 1-0 msimu wa 2021/22 hivyo wana kazi ya kusaka ushindi.

Nabi amesema kuwa kushindwa kufanya vizuri mchezo wa kirafiki haina maana kwamba wachezaji hawana uwezo ila utulivu unahitajika.

“Ni lazima tuweza kufanya utulivu kwa ajili ya mchezo wetu wa Ngao ya Jamii na kuna mengi ambayo ni yakuweza kufanyia marekebisho.

“Kikubwa ni kuona kwamba kila mchezaji anapenda kupata matokeo ile morali bado ipo kwa wachezaji hivyo bado tunaimani yakufanya vizuri mchezo wetu ujao,” amesema Nabi.