KOCHA WA SIMBA KUIBUKIA KWA MKAPA

PABLO Franco, raia wa Hispania leo Novemba 11,2021 anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaoshuhudia mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya DR Congo.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jiono huku timu zote mbili hesabu kubwa ikiwa ni katika kupata ushindi ili kuweza kupata pointi tatu muhimu.

 

Baada ya kuwasili jana Novemba 10,2021 akitokea nchini Hispania moja kwa moja alipelekwa kambini kuweza kuonana na wachezaji pamoja benchi la ufundi ikiwa ni pamoja na Hitimana Thiery na Seleman Matola ambao ni makocha wasaidizi.

 

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez alimkabidhi Pablo jezi ya Stars na kumuambia kwamba anaamini atakuwa miongoni mwa wale watakaokuwa Uwanja wa Mkapa.

Kuhusu hilo Pablo aliweka wazi kuwa anaona fahari kukabidhiwa uzi wa Stars pamoja na kuweza kwenda uwanjani kwa ajili ya kuishuhudia timu ya taifa.