UZI MPYA SIMBA KUTAMBULISHA,SIMBA DAY KUWA YA KIPEKEE

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa tamasha la Simba Day mwaka huu litakuwa la kipekee tofauti na zama.

Ahmed Ally,Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya Simba ameweka wazi kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

Tayari wageni wao ambao ni St George wamewasili Tanzania kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa Agosti 8,2022 Uwanja wa Mkapa.

Pia leo Agosti 7 Simba wanatarajia kutambulisha uzi wao mpya utakaotumika msimu wa 2022/23.

“Wageni wetu St George wameshafika na tunaamini kwamba ni mwendelezo mzuri kuelekea kilele cha Simba Day.

“Itakuwa ni siku ya kipekee na tofauti kabisa na matamasha mengine ambayo yamepita na tunakwenda kufanya jambo kubwa na litkaloacha alama,” amesema.

Kwenye tamasha hilo wanatarajiwa kutambulishwa wachezaji wapya na wale ambao walikuwa na kikosi hicho kwa msimu uliopita.

Miongoni mwa wachezaji wapya ni pamoja na Nassoro Kapama,Habib Kyombo, huku wale waliokuwa msimu uliopita ni pamoja na Henock Inonga,John Bocco.

Tamasha hilo linatimiza mwaka wa 13 baada ya kuanzishwa na muasisi wake ni Mzee Hassan Dalali.