>

AZAM FC YAPOTEZA MCHEZO WAKE WA KIRAFIKI MISRI

OFISA Habari wa Azam FC,Zakaria Thabit amesema kuwa wamepoteza mchezo wa kwanza wakiwa nchini Misri.

Baada ya ubao kusoma Wadi Degla 1-0 Azam FC ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kirafiki,.

Timu hiyo imeweka kambi nchini Misri ikiwa ni maandaizi kwa ajili ya msimu wa 2022/23 ambao unatarajiwa kuanza Agosti.

Thabit amesema kuwa ulikuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa ambapo ameongeza kuwa kizuizi kilikuwa ni mwamba wa goli la wapinzani kwani nafasi ya Idd Chilunda iliishia hapo.

“Ulikuwa ni mchezo mzuri na tulijitahidi kuweza kutafuta bao la kusawazisha kizuizi ilikuwa ni mwaba wa goli la wapinzani kwa kuwa hapo mipira ya wachezaji wetu iliweza kugotea hapo.

“Lakini ni mchezo ambao umetufanya tuweze kujua namna gani tutakuwa na kikosi imara zaidi kwa ajili ya kuleta ushindani,” amesema.