KAZI bado inaendelea kwa walima Zabibu, Dodoma Jiji baada ya leo Julai 23,2022 kumtambulisha winga mshambuliaji, Salum Kihimbwa rasta kutoka Mtibwa Sugar.
Nyota huyo anatajwa kupewa dili la mwaka mmoja ni miongoni mwa mastaa ambao walikuwa ndani ya Mtibwa Sugar msimu wa 2021/22 na wakatimiza lengo la timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kupitia hatua ya mtoano.
Mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya Dodoma Jiji alikuwa ni Collins Opare huku wengine ambao wamesajiliwa ni pamoja na Daniel Mgore, Jimmy Shoji, Amaan Kyata, Christian Zigah, Hassan Mwaterema, Paul Peter.
Wengine ni Rashid Chambo, Randy Bangala na Mwana Kibuta huku ikibakiza wachezaji wasiozidi watatu kufunga usajili wa dirisha kubwa.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa bado kazi inaendelea na wanasajili kwa lengo la kuwa na timu imara msimu wa 2022/23.