KIUNGO mshambuliaji wa Manchester City, Jack Grealish ametabiri kuwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Erling Haaland hatakamatika katika msimu wake wa kwanza ndani ya Premier.
Nyota huyo mwenye miaka 22 ameonekana kuwa karibu sana na Grealish baada ya kujiunga na kikosi hicho akiwa kwenye wiki ya kwanza ya mazoezi nchini Marekani.
‘Erling anaonekana yupo vizuri mazoezini na atakapokuwa fiti kwa asilimia zote atakuwa hakamatiki,” amesema.
Nyota huyo yupo chini ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola ambaye alikiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2021/22.