ALIOU CISSE,KOCHA BORA CAF

ALIOU Cisse, amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Aliou Cisse, 46, aliiongoza Senegal kushinda kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon, mapema mwaka huu, baada ya kuishinda Misri kwa mikwaju ya penalti.

Pia ameiongoza Simba wa Teranga kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka huu mbele ya Misri katika mechi ya mchujo.

Nyota huyo wa zamani mwenye uwezo mkubwa wa kuinoa timu amekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa tangu 2015 na aliiongoza kutinga fainali ya AFCON mwaka 2019 kabla ya ushindi wao mwaka huu.

Aliiongoza Senegal kama nahodha kwenye kombe la dunia la 2002 huko Japan, ambapo Senegal ilifika robo fainali ya kihistoria, ilikuwa ni bora zaidi kuliko taifa lolote la Afrika kuwahi kufika kwenye michuano hiyo.